Pambano La Kusisimua Litarindima Ruangwa –
- March 14, 2025
Mabondia wakali watakutana kwenye pambano la kipekee litakalofanyika Ruangwa katika sherehe za Eid Pili, ikiwa ni ushirikiano wa Mopao Entertainment Promotion na PMBET. Pambano hili linatarajiwa kuwa na mapigano ya kusisimua, ambapo wakali wa sekta ya ngumi, akiwemo Karim Mandonga na Said Mbelwa, watakuwa sehemu ya mashindano haya ya kihistoria.
Mbali na Mandonga na Mbelwa, pambano hili pia litashirikisha mabondia wengine wakali kutoka Ruangwa na mikoa mingine, kuhakikisha shabiki wa ngumi wanapata burudani ya kipekee.
Tunaalikwa kusherehekea Eid Pili kwa pambano la aina yake litakalofanyika kwa staili na ladha ya kipekee, huku mashabiki wakifurahia mapambano ya ngumi yenye ushindani wa hali ya juu. Huu ni wakati wa kuungana na kupongeza mashindano haya na kuwa sehemu ya historia ya ngumi katika Ruangwa!